In Summary
  • Wenger aliachana na Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita baada ya miaka 22 ya utawala wake

LONDON,ENGLAND.BAADA ya Kocha Arsene Wenger kusema ameshapumzika vya kutosha na sasa anataka kuanza kazi ya kufundisha, tayari amezushiwa kuwa anataka kutua AC Milan.

Ripoti kutoka Italia zilisema Wenger alishaanza mazungumzo ya awali na Milan, na anataka kuanza maisha ya soka.

Wenger aliachana na Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita baada ya miaka 22 ya utawala wake Emirates

Mara kwa mara amekuwa akisisitiza alikuwa na mpango wa kurudi kwa kasi kwenye soka, lakini akakanusha habari alikuwa kwenye mpango wa kutua Milan. “Kitu pekee ninachoweza kusema hizo habari si za kweli,” alisema.

“Endapo itatokea, nitawataarifu wote nafsi yangu imetua wapi. Kwa sasa ni uongo ni uvumi tu, hizo habari si za kweli,” Wenger aliiambia BEIN Sports. ‘Siwezi kuzungumzia suala la uvumi, nataka kusema kile ambacho ninakiamini. Taarifa hizo si za kweli.”

ADVERTISEMENT