In Summary

Mashindano hayo yamekuwa yakihusisha vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu nje na ndani ya Tanzania.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mashindano ya michezo kwa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu, mwaka huu.
Mashindano hayo yatafanyika mkoani Dodoma mwezi ujao ambapo zaidi ya vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu 50 kutoka nje na ndani ya Tanzania vitashiriki.
"Na bahati nzuri sana uteuzi wa mgeni rasmi umezingatia na mambo ya nyuma ambapo Mheshimiwa Majaliwa mwenyewe mwaka 1994 hadi 1998 alikuwa ni mmoja wa makocha wa timu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam," alisema Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezo ya Vyuo Vikuu (TUSA), Noel Kihunsi.
Meneja masoko wa Taasisi ya Shadaka inayoratibu mashindano hayo, Sandra Ramadhan Nassib alisema taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha mashindano hayo yanakuwa na mvuto wa aina yake.
 "Mwaka huu tunataka kutengeneza kitu cha tofauti na kile tulichokizoea miaka yote. Hatutaki watu washiriki kwenye michezo tu. Tunataka kila mtu ashiriki kwa nafasi yake. Awe mwanamichezo au asiwe," alisema Sandra.

ADVERTISEMENT