In Summary

Mwili wa Ruge Mutahaba ulipokeleea jana Jumapili mjini Bukoba na mazishi yake yanatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri, Wabunge na Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Bukoba.Mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds, Ruge Mutahaba yatahudhuriwa na vigogo zaidi ya kumi wakiwemo Mawaziri, Wabunge na Wakuu wa Mikoa.

Ratiba iliyotolewa leo Jumatatu asuhuhi, inawataja baadhi ya vigogo hao kuwa ni Hamis Kigwangala (Maliasili na Utalii), Dotto Biteko (Nishati), January Makamba(Mazingira), Angela Kairuki (Uwekezaji) na Juma Aweso (Naibu Waziri wa Maji).


Pia, Wabunge wanaotajwa kwenye ratiba hiyo ni Nape Nnauye (Mtama- CCM), Ridhiwani Kikwete (Chalinze CCM), Aieshi Hilary (Sumbawanga Mjini-CCM) na Wabunge wote wa Mkoa wa Kagera na Wakuu wa Wilaya.


Aidha, mazishi ya Ruge yatahudhuriwa na Wakuu wa Mikoa ya Simiyu, Mwanza, Mara na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Oseah Ndagala.


Tukio la kumuuaga Ruge katika viwanja vya Gymkhana ilikuwa lianze majira ya saa nne asubuhi lakini limechelewa kutokana na mvua inayoendelea kunyesha mkoani hapa.

ADVERTISEMENT