In Summary
  • Waingereza 49, wametajwa kuwania Ballon d’Or huko nyuma. David Beckham, mara 10, anafuatiwa na Sir Bobby Charlton na Wayne Rooney (mara tisa), Bobby Moore (mara saba),   Steven Gerrard, Michael Owen na Jimmy Greaves (mara sita).

Kama hujui, basi ni hivi, Stanley Matthews, ndiye aliyekuwa mshindi wa tuzo ya kwanza ya Ballon d’Or, ya mwaka 1956.

Inafahamika pia Mbrazili Kaka ndiye mwanasoka wa mwisho kushinda tuzo hiyo kabla ya kuanza kwa ufalme wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi waliotamba kwa miaka 10 kabla ya fundi wa mpira wa taifa la Croatia, Luka Modric kuja kumaliza utawala huo kwa kubeba kwa mwaka huu wa 2018. Katika kuonyesha ukongwe wa tuzo hizo, hivi hapa vijimambo unavyopaswa kufahamu kuhusu Ballon d’Or.

Waingereza 49, wametajwa kuwania Ballon d’Or huko nyuma. David Beckham, mara 10, anafuatiwa na Sir Bobby Charlton na Wayne Rooney (mara tisa), Bobby Moore (mara saba),   Steven Gerrard, Michael Owen          na Jimmy Greaves (mara sita).

 Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanaongoza kwa kutwaa tuzo hii mara nyingi. Mara tano. Wanaofuatia ni Michel Platini, Johan Cruyff      na Marco van Basten (mara tatu).

 Tuzo za mwaka huu, ndio tuzo ya kwanza iliyomshuhudia Muargentina Lionel Messi, akimaliza nje ya tatu bora, tangu Mwaka 2006, na alifungana na John Terry na Luca Toni, katika nafasi ya 20. Hii inamaanisha, Messi anaongoza kwa kuingia tatu bora ya tuzo hizo. Ameingia mara 11, Ronaldo   anafuata akiwaamepanda kwenye jukwaa mara saba.

 Shirikisho la soka la Ufaransa (FFF), lilianza kuchapisha majina ya washindi kabla ya mwaka 1995, wakati ambapo wachezaji kutoka Ulaya tu ndio waliokuwa na haki ya kushinda tuzo hii. Kama sio hilo, basi Pele angekuwa na tuzo saba, huku Garrincha, Mario Kempes, Diego Maradona, wangekuwa nazo mbili na Romario moja.

 Tuzo mbili tu za Ballon d’Or, ndizo zilizowahi kuwa na washiriki wa tatu bora kutoka taifa moja. Ni Ujerumani mwaka 1981 (Rummenigge, Breitner, Schuster), kabla ya Waholanzi Van Basten, Gullit na Rijkaard, kuchuana tatu bora mwaka 1988.

Tuzo tatu tu za Ballon d’Or ndizo zilizoshuhudia wanasoka watatu kutoka klabu moja wakiingia tatu bora. AC Milan ilianya hivyo mara mbili, Mwaka 1988 (Van Basten, Gullit, Rijkaard) na Mwaka 1989 (Van Basten, Baresi, Rijkaard). Mwaka 2010, Barcelona (Messi, Xavi, Iniesta).

Ujerumani na Uholanzi, ndio mataifa mawili yanayoongoza kwa kutoa washindi wa Ballon d’Or. Zimetoa washindi mara saba, kila mmoja. Ufaransa na Ureno, zinashika nafasi ya pili (washindi sita), Italia, Brazil, England na Argentina, zikifungana katika nafasi ya tatu (washindi watano).

 Liberia wamefungana na Northern Ireland na Scotland kwa kutoa mshindi mmoja.

 Barcelona inaongoza vilabu vilivyotoa washindi mara nyingi (11), Real Madrid ni ya pili (10), Juventus na AC Milan wanafungana nafasi ya tatu (8).

Blackpool na Dukla Prague wametoa idadi ya washindi sawa na Liverpool (mshindi), na idadi kubwa zaidi ya Arsenal, ambayo haijawahi kuwa na mchezaji aliyeshinda tuzo hii.

 George Weah ni mchezaji pekee, asiye na uraia wala damu ya Bara laUlaya, ambaye amewahi kushinda tuzo na anasalia kuwa Mwafrika pekee, ambaye amewahi kushinda tuzo ya Ballon d’Or.

 Paul Scholes anaongoza kwa kutoambulia kura hata moja kwenye Ballon d’Or, licha ya kuteuliwa zaidi ya mara tano.

Kabla ya uteuzi wa Harry Kane, kwenye tuzo hizi (2017 na 2018), Jamie Vardy, alikuwa Muingereza pekee ambaye alipata bahati ya kuteuliwa kuwania tuzo hii, tangu mwaka 2012.

Lev Yashin, raia wa Soviet, ndiye Kipa pekee amabye amewahi kutwaatuzo hii. Alitwaa tuzo ya Mwaka 1963.

 Fabio Cannavaro, raia wa Italia, ndiye beki pekee ambaye amewahi kutwaa tuzo hii, tangu mwaka 1996.

Jimmy Greaves, ndiye mchezaji pekee ambaye amewahi kutwaa tuzo ya Ballon d’Or, mwaka ambao amechezea vilabu vitatu tofauti (Chelsea, Milan na Tottenham). Alitwaa tuzo hiyo, Mwaka 1961.

John Jensen, ndiye mchezaji pekee aliyefunga idadi ya mabao ambayo ni sawa na idadi ya uteuzi aliopata kuwania tuzo ya Ballon d’Or. Wakati akiteuliwa, nyota huyu wa zamani wa Arsenal, alikuwa amefunga bao moja tu, katika mechi 99 za EPL.

Mwaka 2005, Beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher, alipata kura sawa na Cristiano Ronaldo, walipofungana katika nafasi ya 20.

Mwaka 2010, akiwa Sunderland, Mghana Asamoah Gyan, alikuwa mchezaji wa pili anayecheza kwenye EPL, aliyepigiwa kura nyingi katika uteuzi wa tuzo za Ballon d’Or.

 Cardiff (Ivor Allchurch, mwaka 1965), Scunthorpe (Ken Jones, mwaka 1959) na QPR (Don Givens, mwaka 1975), zinafungana katika idadi yakutoa wachezaji walioteuliwa kuwania tuzo za Ballon d’Or. Walitoa mchezaji mmoja, kila mmoja.

 

ADVERTISEMENT