In Summary

Teknolojia ya Video Assistant Referee, mfumo wa video unaomwezesha mwamuzi kupitia kwa kutezama matukio mbalimbali yanayotokea uwanjani, wakati mechi ikiendelea.

Dar es Salaam. Kiungo wa zamani wa Yanga, Ally Yusuph 'Tigana' amesema wasimamizi wa teknolojia za usaidizi wa video ‘VAR’ kwa waamuzi wakati wa fainali za Afcon wanatakiwa kuwa makini zaidi.

Tigana alisema wasipokuwa makini yanaweza kutokea yale ya kwenye mchezo wa fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mchezo ulivunjika.

“Sina maana kwamba teknolojia ni mbaya ila ni vizuri wahusika wakawa nazo makini ili zisilete utata wa kiuamuzi, naamini lengo la kuletwa kwa VAR ni kuondoa makosa ya kibinadamu. Japo kwa kiasi fulani kuna radha fulani kwenye soka inapungua,” alisema Tigana ambaye mbali na kuichezea Yanga pia aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Tanzania.

Kiungo huyo wa zamani wa Yanga, alisema Taifa Stars inatakiwa kujiandaa vyakutosha ili kwenda kushindana na sio kushiriki katika fainali hizo.

Upande mwingine, Tigana alisema wachezaji wanatakiwa kutumia fursa ya kucheza fainali hizo kubwa duniani kujitangaza ili wasajiliwe na klabu kubwa ndani na nje ya Afrika.

 

ADVERTISEMENT