In Summary

 

  • Shabiki achekelea kikosi cha Harambee Stars kilichotangazwa majuzi, akisema kitaweza kutuletea matokeo mazuri ya mechi zijazo.

MBONA timu yetu ya Bandari FC imeanza kupunguza makali yake ya kawaida, tunatupa pointi kiholela?

Jacob Mwadime, Likoni

NIMEFURAHIA kikosi cha Harambee Stars kilichotangazwa majuzi, kitaweza kutuletea matokeo mazuri ya mechi zijazo.

Harub Lamteti, Kamkunji

HEKO Bandari Fan Club kwa kufanya Roadshow na kuhamasisha mashabiki wetu wafike kwa wingi kiwanjani.

Saleh Maftah, Lamu

GOR Mahia fanyeni bidii musituangushe, tuna hamu tupate mara ya pili Kombe la barani Afrika.

George Odipo, Kibera.

NINA imani kubwa Chelsea tutapanda ngazi na kumaliza Top Four.

Sophia Clara, Malindi.

NAWAOMBA mashabiki wa soka wafurike viwanjani kuinua klabu zetu badala ya kushabikia timu za England.

Jacob Mudavadi, Malaba.

NI hamu kubwa ya timu yangu ya Liverpool ishinde taji la Ligi Kuu ya Uingereza.

Abubakar El-Maawiy, Mazeras.

NATABIRI si Liverpool au Man City itakayobeba Kombe la EPL bali ni Tottenham ama Man United.

Asha Saumu, Taru

NAWASHUKURU Mwanaspoti kwa kutoa habari za wasanii chipukizi wa Mkoa wa Pwani nao watambulike.

DJ Maarufu, Voi.

NI lini timu yangu ya Nzoia Sugar itaweza kubeba taji la Ligi Kuu?

Solomon Kweku, Bungoma.

NAWAPONGEZA Mathare United FC kwa kufanikiwa kuondoka na pointi moja Mombasa baada ya sare tasa na Bandari FC.

Stella Maina, Mathare Nairobi.

 

 

 

 

ADVERTISEMENT