In Summary

Gor Mahia timu ambayo aliichezea straika wa Simba, Dan Sserunkuma tayari imetoa ofa kwa Kwizera raia wa Burundi ambayo amekubaliana nayo na kilichobaki ni kusaini mkataba huo na kuanza kazi baada ya kutemwa na Simba katika usajili wa dirisha dogo mwezi uliopita.

KWELI kila mtu na bahati yake, kwani kiungo aliyetemwa na Simba, Pierre Kwizera anaondoka nchini kesho Jumanne kwenda kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Gor Mahia ya Kenya inayoshiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Gor Mahia timu ambayo aliichezea straika wa Simba, Dan Sserunkuma tayari imetoa ofa kwa Kwizera raia wa Burundi ambayo amekubaliana nayo na kilichobaki ni kusaini mkataba huo na kuanza kazi baada ya kutemwa na Simba katika usajili wa dirisha dogo mwezi uliopita.

Mpaka sasa Simba bado haijamlipa fidia kiungo huyo ambaye anaidai Sh10 milioni baada ya kukubali kumlipa fidia ya mishahara ya miezi sita ambapo kwa mwezi alikuwa akilipwa dola 1000 (Sh 1.7Milioni). Jumla anapaswa kulipwa dola 6000 (Sh10 milioni).

Habari za uhakika zilizoifikia Mwanaspoti ni kwamba jana Jumatatu, Kwizera alitarajia kuonana na viongozi wa Simba ili kuandikishana juu ya malipo hayo ambayo yameelezwa amekuwa akizungushwa kila anapowadai.

Akithibitisha juu ya hili, Kwizera alisema: “Ni kweli Gor Mahia wananihitaji tumefanya mazungumzo ya awali ila nitakwenda huko kwa ajili ya kumalizana.”

ADVERTISEMENT