In Summary
  • Vyombo vya habari vya Argentina zimechapisha picha hizo kwa mara ya kwanza na zilipigwa Januari, 1998 kwenye ufukwe wa Atlantic holiday resort mjini Punta Mogotes.

Barcelona,Hispania .ACHANA na staili za wapenzi wengi kukutana kwenye vituo vya usafiri, nyumba za ibada ama shuleni, kwa supastaa wa Barcelona Lionel Messi mambo ni tofauti kabisa unaambiwa.

Messi, ambaye kwa sasa anaogelea kwenye bwawa la mafanikio ya soka duniani akizimiwa na kila shabiki, imefichuka walianza kupata hisia za malovee na mkewe Antonela Rocuzzo tangu wakiwa watoto kabisa. Picha za hivi karibuni zimekuwa gumzo kote duniani baada ya kumwonyesha Messi na Antonela, ambaye ni mama wa watoto watatu: Thiago, Mateo na Ciro wakiwa ufukweni na wanafamilia wengine wakati wakiwa na miaka 10 tu, walipokutana kwenye michezo ya watoto.

Vyombo vya habari vya Argentina zimechapisha picha hizo kwa mara ya kwanza na zilipigwa Januari, 1998 kwenye ufukwe wa Atlantic holiday resort mjini Punta Mogotes.

Wakati huo Messi alikuwa kwenye mashindano ya timu za watoto ya mji jirani wa Balcarce, tayari walishaanza kufahamiana na Antonela.

Hata hivyo, siku hiyo Antonela alikwenda kushuhudia michuano hiyo akiwa na wazazi wake kwa ajili ya kumpa mzuka mpwa wake Lucas Scaglia, ambaye alikuwa akikipiga chama moja na Messi. Katika picha hiyo, wengine waliotajwa mbali na Messi na Antonela ni pamoja na Lucas na Matias Pecce. Imeelezwa, siku ya michuano hiyo wazazi wa Messi, Jorge na Celia waliokuwa wakiishi mjini Rosario umbali wa saa nane kufika Punta Mogotes, walikuwa wakiwapeleka watoto kushiriki michezo hiyo.

Kuibuliwa kwa picha hiyo kulitokana na mawazo ya gazeti moja la Argentina kujaribu kusaka picha za utotoni za mastaa mbalimbali wa nchi hiyo, ambao walikuwa na kawaida ya kwenda kushiriki michezo kwenye eneo hilo na ndipo ikanaswa ya La Pulga.

ADVERTISEMENT