In Summary
  • Kama ilivyo kwa Ronaldo, Pogba alikuwa akijiandaa kucheza na timu yake ya zamani jana usiku wakati United ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Juve katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Old Trafford. Pogba alisema ataona raha kucheza na Ronaldo.

MANCHESTER, England.KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba haishi vituko. Haoni shida kumchanganya kocha wake, Jose Mourinho na wachezaji wenzake.

Kuna wakati aliaga wenzake kuwa sasa safari imeiva anakwenda Barcelona. Wakayamaliza. Ni wakati mmoja, Mourinho alimwambia kama anaona hataki kucheza aandike tu barua, nayo wakayamaliza.

Juzi kawachanganya tena. Kasema atafurahi kama atacheza pamoja na Cristiano Ronaldo Juventus na kuzidisha wasiwasi wa mchezaji huyo kutua mjini Turin.

Ronaldo, winga wa zamani wa Manchester United alijiunga na Juventus akitokea Real Madrid. Safari ya mchezaji huyo kwenda Turin imeonyesha mafanikio kwani hadi sasa amefunga mara saba katika mechi 10 za mashindano yote.

Kama ilivyo kwa Ronaldo, Pogba alikuwa akijiandaa kucheza na timu yake ya zamani jana usiku wakati United ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Juve katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Old Trafford. Pogba alisema ataona raha kucheza na Ronaldo.

“Nadhani ni uamuzi mzuri kumleta kikosini Juventus: Kuwa na Cristiano kunahamasisha kwenye timu, kucheza na mchezaji mkubwa kama yeye, Messi au Neymar ni poa sana.”

ADVERTISEMENT