In Summary

Mwakalebela alisema wachezaji hao sio mwisho wa usajili bali wataendelea na usajili huo kuanzia wiki ijayo.

MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amewatuliza mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwaambia usajili unaendelea.
Mwakalebela aliyasema hayo akiwa anafungua shughuli yao ya Kubwa Kuliko inyaofanyika ukumbi wa Daimond Jubilee huku akiwatambulisha wachezaji kiungo Abdulaziz Makame(Zanzibar) na mshambuliaji Juma Balinya wa Uganda.
Mwakalebela alisema wachezaji hao sio mwisho wa usajili bali wataendelea na usajili huo kuanzia wiki ijayo.
"Tunaendelea kusajili, wiki ijayo nadhani shughuli ya usajili itaendelea, wana Yanga muwe na amani kabisa," alisema.
Wachezaji waliosajiliwa Yanga mpaka hivi sasa ni Issah Bigirimana, Abdulaziz Makame, Juma Balinya, Lamine Moro na Patrick Sibomana.

ADVERTISEMENT