In Summary

Uwanja wa Samora umekuwa na changamoto ya kujaa maji mara kwa maa na kufanya timu zisalie kwa siku zaidi katika uwanja huo ili kuweza kucheza mechi zao.

MECHI ya Lipuli dhidi ya JKT Tanzania iliyotakiwa kuchezwa jioni leo saa kumi, imehairishwa baada ya uwanja wa Samora kujaa maji.
Kupitia kwa msemaji wa timu hiyo, Jamila Mtabazi, alithibitisha kwamba mechi hiyo imeghairishwa na itachezwa kesho baada ya uwanja kwa sio rafiki.
"Mechi yetu dhidi ya Lipuli haipo tena kwasababu uwanja umejaa maji, hivyo itachezwa kesho hapa hapa jioni," alisema.
Uwanja wa Samora umekuwa na changamoto ya kujaa maji mara kwa maa na kufanya timu zisalie kwa siku zaidi katika uwanja huo ili kuweza kucheza mechi zao.

ADVERTISEMENT