MSANII wa mziki wa dansi, Muumini Mwinjuma ameibukia katika hafla ya Kubwa Kuliko iliyoandaliwa na klabu ya Yanga kwaajili ya kuchangia pesa.
Mwinjuma alipanda jukwaani na Chaz Baba na kuanza kutumbuiza kiasi cha kuwafanya wanachama wa Yanga waliokuwepo ukumbini hapa kushangilia kwa shangwe.
Wasanii hao waliimba nyimbo mbalimbali ikiwemo 'Nampenda Kuliko Wote' ambayo iliibua shangwe ukumbini hapa.
WOLPER, DOKII NDANI
Wasanii wa maigizo Jackline Wolper na Dokii nao ni miongoni mwa wanachama wa Yanga waliofika kwenye hafla hiyo.
Wasanii hao walitambulishwa na kusimama lakini kubwa kuliko ilikuwa kwa Dokii baada ya msanii huyo kujitambulisha kama mke wa Mzee Hamisi Kilomoni.
Mzee Kilomoni hivi sasa amezua utata katika klabu ya Simba baada ya kudai timu hiyo haiwezi kuwa chini ya Mwekezaji Mohammed Dewji 'Mo Dewji' ambapo Kilomoni ndiye anayedaiwa kushikilia hati miliki ya jengo la Simba lililopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo, jijini Dar es Salaam..

ADVERTISEMENT