In Summary
  • Akizungumza na Mwanaspoti, Katwila alisema amepitwa alama saba Simba waliopo nafasi ya tatu katika msimamo japo ine michezo kadhaa mkononi, lakini anaamini wakikomaa wafanya vema mbele ya safari kabla msimu haujamalizika.

MTIBWA Sugar imetoka kulazimishwa sare ya 1-1 na African Lyon nyumbani, lakini sasa unaambiwa benchi la ufundi la timu hiyo licha ya kukiri matokeo mabaya yanawaumiza, lakini mipango yao ni kumaliza kwenye Tano Bora mwisho wa msimu huu.

Mtibwa ipo nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi ikiwa imecheza michezo 21 na kushinda nane, ikipoteza nane na kutoka sare tano ikiwa imefungwa mabao 20 na kufungwa 29, lakini Kocha Zubeiry Katwila alisema kuachwa nyuma na wapinzani waliopo kileleni, lakini bado anaimani timu yake itamaliza Tano Bora.

Akizungumza na Mwanaspoti, Katwila alisema amepitwa alama saba Simba waliopo nafasi ya tatu katika msimamo japo ine michezo kadhaa mkononi, lakini anaamini wakikomaa wafanya vema mbele ya safari kabla msimu haujamalizika.

“Mtibwa bado ina nafasi kwani hatujaacha sana na timu zilizopo juu yetu, ukiondoa Yanga na Azam, hivyo naamini tukikaa vyema hadi mwisho msimu ni lazima tuwe kwenye Tano Bora kwani hapo panatutosha baada ya kupoteza dira ya kuwania ubingwa,” alisema Katwila.

Akizungumzia sababu kubwa za kikosi chache kupoteza pointi katika michezo ya hivi karibuni, alisema ni ugumu wa duru la pili, huku akisisitiza mechi zijazo watapambana kufanya vizuri.

“Lala salama, kila timu inahitaji pointi kutoka kwa mpinzani wake na kuongeza kuwa ubora wa timu ndio unajulikana na huwa hainaga uwanja wa nyumbani au ugenini kila timu inakuwa inahitaji kubaki Ligi Kuu, lakini bado hatujakata tamaa nasi wamo bwana,” alisema kocha huyo.

ADVERTISEMENT