In Summary

Tanzania imecheza mechi mbili za kirafiki ikifungwa na Misri 1-0, kabla ya kulazimisha sare 1-1 na Zimbabwe sasa inajianda na Afcon itacheza mechi ya kwanza Juni 23 dhidi ya Senegal.

Dar es Salaam. Baada ya Taifa Stars kulazimisha sare 1-1 na Zimbabwe jana usiku kocha msaidizi Hemed Morocco amesema wamefanikiwa kupunguza mapungufu mengi yaliyojitokeza katika mechi dhidi ya Misri.

Kocha Morocco alisema kwa jinsi alivyocheza ni imani yao kikosi kitakuwa tayari katika mechi ya kwanza dhidi ya Senegal.

"Timu zote zimekuja kushiriki mashindano haya ni ngumu kwa maana hiyo hizi mechi mbili ambazo wamecheza za kirafiki ni kipimo sahihi kuelekea katika mechi za kimashindano kwani watakuwa wamefahamu ubora na mapungufu ya kikosi cheo ambayo watakuwa wameyafanyia kazi,' alisema Morocco.

"Kikubwa wamerekebisha makosa na kuboresha ubora wa sehemu ambazo wamekuwa wakifanya vizuri katika mechi zote hizi mbili na matumaini watakwenda kufanya hivyo kwenye mashindano."

Baada ya mchezo huo kiungo wa zamani wa Yanga, Zimbabwe, Thabani Kamusoko alisema mechi ilikuwa ngumu kutokana timu zote zimejiandaa vizuri, lakini nashukuru Mungu na nimejisikia furaha kukutana na ndugu zangu ambao nimeishi nao kwa muda mrefu nikiwa na cheza soka Tanzania katika timu ya Yanga.

"Ugumu wa mechi na mpaka kumalizika kwa sare ulitokana na maandalizi ya timu zote mbili kujindaa vizuri kuelekea katika mashindano hayo huku wakiwa na malengo ya kufanya vizuri," alisema Kamusoko.

ADVERTISEMENT