In Summary
  • Ronaldo na Messi ni wachezaji pekee ambao kila mmoja amenyakuwa tuzo tano za mwanasoka bora wa mwaka wa Fifa.

Barcelona, Hispania. Lionel Messi amemwagia sifa Cristiano Ronaldo baada ya kuonyesha kiwango cha juu na kuisaidia Juventus kufuzu kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Messi baada ya kuonyesha kiwango cha juu dhidi ya Lyon na kufunga mabao mawili katika ushindi wa Barcelona wa mabao 5-1, alisema alichokifanya Ronaldo ni kitu cha kipekee.

Messi alisema: 'Nafikiri kilichotokea kwa Cristiano na Juventus ni jambo la kushangaza. Nilikuwa nafikiri labda Atletico wangekuwa bora zaidi, lakini Juventus iliwabadilisha na miujiza ya Cristiano katika usiku huu yalizaa mabao matatu.'

Mchambuzi Chris Sutton naye alikiri kuwa kiwango cha Ronaldo katika usiku wa Jumanne kilikuwa cha kipekee.

Alizungumza jinsi gani Juventus wanaweza kubadilisha matokeo baada ya mchezo wa kwanza dhidi ya Atletico Madrid waliofungwa 2-0, kabla ya Ronaldo kupindua meza kwa kufunga mabao matatu jijini Turin.

Sutton alisema: 'Yupo Juventus kwa lengo la kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa. Nilikuwa nafikiri Juventus tayari wameshatoka baadaya matokeo ya jijini Madrid, lakini Ronaldo ameibeba Juventus.'

ADVERTISEMENT