In Summary

Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya tatu kwa Marsh kwenye uwanja wa Nyamagana na wa nne katika Ligi sawa na wapinzani wao ilishuhudiwa kila upande ukiondoka na alama moja moja.

Mwanza.Mzimu wa sare nyumbani umeendelea kuitafuna Marsh Queen baada ya jana Jumatano kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mapinduzi Queen katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake.
Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya tatu kwa Marsh kwenye uwanja wa Nyamagana na wa nne katika Ligi sawa na wapinzani wao ilishuhudiwa kila upande ukiondoka na alama moja moja.
Marsh Queen ndio walitangulia kupata bao dakika ya 25 kupitia kwa Mwanvita Muba,bao lililosawazishwa dakika ya 38 na Winfrida Mnyali.
Hata hivyo timu zote zitajilaumu kwa nafasi nyingi za wazi ilizokosa na kusababisha matokeo hayo ndani ya dakika 90.
Kwa matokeo hayo Marsh wanafikisha pointi tano huku Mapinduzi wakifikisha alama moja baada ya kila timu kucheza michezo minne.

ADVERTISEMENT