In Summary

 

  • Manchester City imefikisha pointi 41 huku ikiiacha Manchester United kwa jumla ya alama 19 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

England. Ushindi wa Manchester City dhidi ya Watford wa mabao 2-1 jana Jumanne umeiongezea presha Manchester United kuelekea mechi yake ya leo Jumatano kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Ushindi wa Manchester City uweongeza tofauti ya pointi na wapinzani wao Manchester United baada ya kufikisha alama 41 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na kuwafanya kuwa na tofauti ya alama 19.

Man United wataingia uwanjani wakitafuta alama tatu  muhimu ambapo hata hivyo hazitawawezesha kuishusha Arsenal ambayo ina pointi 30.

Man United ikishinda mechi ya leo itafikisha pointi 25  wakati Arsenal iliyopo nafasi ya nne  kabla ya mechi ya leo ana alama 30.

Timu zingine ambazo zilicheza jana Jumanne AFC Bournrmouth iliizidi kete Huddersfield Town ikiilaza mabao 2-1, Brighton & Hove Albion iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Cystal Palace.

West Ham United iliitambia Cardiff City mabao 3-1 huku Watford walipoteza mchezo kwenye uwanja wake wa nyumbani wakilala mabao 2-1 dhidi ya Manchester City.

 

ADVERTISEMENT