In Summary
  • Ushindi huo umewafanya Yanga kurejea kileleni wakiwa na pointi 83 katika michezo 36 waliyocheza, huku Simba wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 82 katika michezo 33 waliyocheza.

KLABU ya Yanga imefanikiwa kurejea katika nafasi ya kwanza baada ya kuichapa Ruvu Shooting bao 1-0 katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Ushindi huo umewafanya Yanga kurejea kileleni wakiwa na pointi 83 katika michezo 36 waliyocheza, huku Simba wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 82 katika michezo 33 waliyocheza.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kukatana shoka, Yanga waliweza kutumia makosa machache ambayo yaliweza kuipa ushindi mbele ya Shooting.

Mwanaspoti linakuletea uchambuzi mfupi namna ambavyo Yanga walivyoweza kupata ushindi huo na kurejea kileleni na kuishusha Simba.

KUTOKATA TAMAA

Licha ya kwamba Yanga imekua ya kuunga unga huku mashabiki wao wenyewe wakiwa wanalitambua hilo, kwa upande wa wachezaji wao hawajawahi kukata tamaa.