In Summary
  • Kundi hilo la wachezaji 23 wa Ivory Coast linatarajia kuingia kambini huko Abu Dhabi ambako pia itacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Uganda, Juni 14 na baadaye Ethiopia, Juni 18.

MABAO mawili ambayo mshambuliaji mkongwe wa Ivory Coast, Wilfried Bony aliyafunga kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Comoro, Ijumaa iliyopita yamempa tiketi ya kushiriki fainali za Afcon zitakazochezwa Misri wiki mbili zijazo.

Bony (31) ndiye mchezaji pekee kwenye kikois cha Ivory Coast ambaye hana timu kwa sasa lakini kiwango bora alichoonyesha dhidi ya Morocco kimemshawishi Kocha Ibrahim Camara kumjumuisha kwenye kundi la wachezaji 23 watakaoshiriki Afcon.

Kama ilivyotegemewa, Camara amewajumuisha pia baadhi ya mastaa wanaotamba kwenye klabu mbalimbali Ulaya.

Kundi hilo la wachezaji 23 wa Ivory Coast linatarajia kuingia kambini huko Abu Dhabi ambako pia itacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Uganda, Juni 14 na baadaye Ethiopia, Juni 18.

Kikosi hicho cha mwisho cha Ivory Coast kinaundwa na makipa Sylvain Gbohouo (TP Mazembe), Ali Badra (Free State Stars), Tape Ira (FC San Pedro) wakati mabeki ni Serge Aurier (Tottenham), Wilfried Kanon (ADO The Hague), Wonlo Coulibaly (ASEC Mimosas), Ismaël Traoré (Angers), Mamadou Bagayoko (Red Star), Cheikh Comara (Wydad Casablanca) na Souleyman Bamba (Rennes).

Viungo ni Jean-Philippe Gbamin (Mainz), Geoffrey Serey Dié (Neuchâtel Xamax), Jean-Michaël Seri (Fulham), Victorian Angban (Metz), Franck Kessié (AC Milan) na Ibrahim Sangaré (Toulouse) wakati washambuliaji ni Max-Alain Gradel (Toulouse), Nicolas Pépé (Lille), Wilfried Zaha (Crystal Palace), Jonathan Kodjia (Aston Villa, England), Roger Assalé (Young Boys), Maxwel Cornet (Lyon) na Wilfried Bony (huru).

ADVERTISEMENT