In Summary

Washindi hawa wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo wiki iliyopita

MCHEKESHAJI na Mc maarufu nchini, Mc Pilipili amenogesha ugawaji zawadi katika droo iliyochezeshwa na Mwalimu Commercial Bank.
Pilipili alifika katika bank na kuamua kufungua baada ya kukoshwa na muenendo wa droo zilizofanyika katika kutafuta mshindi.
"Mimi nilikuwa mwalimu huko nyuma lakini niliachana nayo kazi ile na sasa nipo katika kazi nyingine, nimeamua kufungua akaunti hapa kwasababu droo zake zinafanyika kwa wazi na hii ni bank ya wote," alisema.
Wakati huo huo mshindi wa Laki Tano na Bodaboda, Mwalimu Goden Mdinda, alisema ni jambo kubwa alilopata baada ya droo hiyo kufayika.
"Nimchukua zawadi mbili baada ya kuchezeshwa droo, nawashauli watu wengine nao wajiunge ili waweze kujishindia kama ilivyokuwa kwangu,'' alisema.
Naye Tatu Lyimo aliyejishindia Shilingi Laki Tano baada ya kuchezeshwa droo hiyo,  amesema amejishindia zawadi hiyo licha ya kwamba yeye sio mwalimu hivyo ni jambo ambalo ni la kweli.

ADVERTISEMENT