In Summary
  • Siku chache zilizopita, Simiyu alitua nchini akitokea Kenya kwa lengo la kufanya usajili wa wachezaji wawili kwenye nafasi ya golikipa na beki wa kushoto.

MENEJA wa KCB FC, Bramweli Simiyu amefunguka juu ya usajili walioufanya kwa wachezaji wawili wa Kitanzania na kusema, Peter Manyika na Jamal Mwambeleko wanaweza kuisaidia timu hiyo kumaliza kwenye nafasi nne za juu kwenye ligi.

Siku chache zilizopita, Simiyu alitua nchini akitokea Kenya kwa lengo la kufanya usajili wa wachezaji wawili kwenye nafasi ya golikipa na beki wa kushoto.

“Tunaufahamu uwezo wa Manyika kwa sababu alifanya vizuri kipindi kile kwenye mashindano ya Sportpesa yaliyofanyika kwetu Kenya kwa hiyo ni aina ya mchezaji ambaye ataenda na mikakati yetu. Mwambeleko naye ni mchezaji mzuri,” alisema Simiyu.

ADVERTISEMENT