In Summary
  • Timu hizo mbili Barca na Atletico zitapaswa kukubaliana juu ya mambo ya ada ya uhamisho na mchezaji huyo dau lake litashuka na kufikia Euro 125 milioni itakapofika Julai Mosi mwaka huu kutokana na kipengele kilichowekwa kwenye mkataba wake.

BARCELONA, HISPANIA . MABOSI wa Atletico Madrid wanaamini supastaa wao Antoine Griezmann ataondoka kwenye kikosi hicho mwishoni mwa msimu huu baada ya kufikia makubaliano binafsi na Barcelona.

Huko Hispania kumekuwa na ripoti Atletico wameshafahamu vita wanayokwenda kupambana kumbakiza Griezmann kwenye kikosi chao watashindwa tu kwa sababu mchezaji mwenyewe ameshakubaliana kila kitu na Barcelona.

Taarifa za kuhusu jambo hilo zilibainisha:

“Atletico tayari wameshafahamu Griezmann ameshakubaliana na Barcelona. Dili limeshakwisha.”

Timu hizo mbili Barca na Atletico zitapaswa kukubaliana juu ya mambo ya ada ya uhamisho na mchezaji huyo dau lake litashuka na kufikia Euro 125 milioni itakapofika Julai Mosi mwaka huu kutokana na kipengele kilichowekwa kwenye mkataba wake.

Kwa mujibu wa SER, wiki hii kunatarajiwa kuanza mikutano ya viongozi wa pande hizo mbili ili kukamilisha dili.

ADVERTISEMENT