In Summary
  • Bosi wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge, wanatafuta mchezaji wa kwenda kuziba pengo la mawinga Franck Ribery na Arjen Robben walioachana na timu hiyo. Chaguo lao la kwanza wababe hao wa Bundesliga kwenye jambo hilo ni kumsajili, Leroy Sane.

MUNICH, UJERUMANI. BAYERN Munich wamesema kwamba hawajafuta mpango wao wa kumsajili Leroy Sane na kwamba watadili naye baada ya likizo kumalizika na jambo hilo litawafanya waachana na staa wa Chelsea, Callum Hudson-Odoi.

Mchezaji huyo wa Chelsea mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu ujao, lakini Bayern Munich walikumbana na wakati mgumu walipotangaza ofa ya kumchukua, ambapo dau lao la Pauni 35 milioni lilikataliwa na wababe hao wa Stamford Bridge.

Kocha mpya wa The Blues, Frank Lampard amesema tena kwa msisitizo kwamba Hudson-Odoi anapaswa kubaki Stamford Bridge kwa sababu anataka kumtengeneza ili awe mchezaji wa kiwango cha dunia.

Wiki iliyopita iliripotiwa kwamba mchezaji huyo atakuwa na furaha na kusaini mkataba mrefu wa kuichezea timu hiyo kama atapewa uhakika wa nafasi ya kucheza kwenye kikosi.

Bosi wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge, wanatafuta mchezaji wa kwenda kuziba pengo la mawinga Franck Ribery na Arjen Robben walioachana na timu hiyo. Chaguo lao la kwanza wababe hao wa Bundesliga kwenye jambo hilo ni kumsajili, Leroy Sane.

Lakini, winga huyo wa Manchester City timu yake inamthaminisha kuwa na thamani ya Pauni 90 milioni, lakini Bayern wanaamini baada ya mchezaji huyo kutoka likizo basi watafanya naye mazungumzo ya kunasa huduma yake.

Kocha wa wababe hao, Niko Kovac amedai kwamba bado wanamfuatiliia Hudson-Odoi, lakini watahangaika tu kunasa saini yake kama watalikosa chaguo lao la kwanza ambalo ni Sane.

Niko Kovac alisema: "Atatusaidia sana. Tumeona kwa namna ambavyo amekuwa akifanya na timu ya taifa ya Ujerumani na kwenda timu ya Man City."

Man City wanataka kumpa mkataba mpya winga huyo baada ya huu wa sasa kumaliza miaka miwili.

ADVERTISEMENT