In Summary
  • Licha ya ushindi walioupata katika mchezo wa kwanza, kocha wa Angola bado anataka kuhakikisha anafanya vizuri katika michezo inayofuata.

Dar es Salaam. Kocha wa Angola, Pedro Dos Santos amesema anatengeneza kikosi imara kitakachofanya vizuri katika Fainali za Afcon pamoja na kupata tiketi ya kucheza Kombe la Dunia Brazil.

Akizungumza na Mwanaspoti.co.tz baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda, Dos Santos alisema kikosi chake kinatoa taswira ya kuelekea katika kikosi cha timu ya wakubwa.

“Huku ndio kwenye msingi kwahiyo lazima huku chini patengenezwe vizuri ili kufanya vizuri juu, naamini kabisa kwamba nina kikosi kizuri ambacho kinapambana na kuendelea kufanya hivyo,”.

Aliongeza ushindi walioupata dhidi ya Uganda haujawafanya kulizika badala yake ni kuendelea kupambana vya kutosha ili kukata tiketi ya kwenda katika kombe la Dunia.

“Bado tunatakiwa kupata matokeo katika michezo yetu ijayo, ushindi ndio utatuweka sisi katika sehemu nzuri na sio kitu kingine, licha ya kushinda kuna vitu inabidi tuviongeze,” alisema Dos Santos.

ADVERTISEMENT