In Summary

Algeria mara ya mwisho kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika ilikuwa 1990.

Cairo, Misri. Kocha wa Algeria, Djamel Belmadi amesema malengo yake ni kufanya vizuri zaidi katika fainali za Mataifa ya Afrika pamoja na kuwepo kwa miamba kama Senegal na Morocco.

Algeria imetwaa kwa mara ya mwisho Kombe la Mataifa ya Afrika 1990, mwaka huu imepangwa Kundi C pamoja na Senegal, Kenya na Tanzania.

"Sisi siyo pekee tunaosaka ubingwa huo," Belmadi aliimbia gazeti la Algeria, El-Heddaf jana Jumapili.

"Kuna timu nyingine ambazo zinataka ubingwa huu kama Senegal na Morocco.

"Senegal timu yao haijabadilika kwa miaka mitatu sasa. Sawa na ilivyokuwa kwa Morocco, ambao watakuwa na wachezaji wale wale chini ya kocha wao wa muda mrefu Herve Renard, hiyo ni tofauti na kwetu."

Lakini Belmadi amechukua jukumu la kuifundisha Algeria pale Agosti mwaka jana, amesisitiza kikosi chake kipo tayari kwa kibarua hicho.

"Ni ukweli kuwa Morocco na Senegal wapo katika nafasi nzuri, lakini na sisi tupo tayari kwa mapambano," aliongeza.

"Wachezaji wangu wamejianda kwa Afcon na wapo tayari kuhakikisha tunakwenda mbali zaidi hadi kuchukua ubingwa."

ADVERTISEMENT