In Summary
  • Huku Patty akitoa kauli, Kocha Alvarez kwa upande wake ameamua kusalia kimya kuhusiana na sakata hilo.

KLABU ya soka ya Libertad de Paraguay imeripotiwa kumtimua kazi kocha wake, Leonel Alvarez baada ya kuchepuka na mke wa mchezaji wake.

kwa mujibu wa vyombo vya habari, Alvarez mwenye umri wa miaka 51, amekuwa akitoka kimapenzi kimyakimya na kichuna Patty Gonzalez, ambaye ni mke wa staa wa kikosi chake, Edgar Benitez.

Baada ya taarifa hizo kusambaa, Patty alijitokeza na kukanusha. “Nawahakikishieni sio kweli. Hatuna mazoea kabisa, hivyo inawezekanaje tukawa na uhusiano,” Patty alijitetea.

Huku Patty akitoa kauli, Kocha Alvarez kwa upande wake ameamua kusalia kimya kuhusiana na sakata hilo.

Hata hivyo, wakili wa klabu hiyo, Gerardo Acost alinukuliwa akisema klabu ilichukua hatua ya kumtimua kazi Alvarez baada yake kushindwa kuisimamia timu inavyostahili pamoja na benchi lake la ukufunzi.

ADVERTISEMENT