In Summary

Kwa mwaka jana boomplay ilizalisha nyimbo milioni 833 na takribani nyimbo 30,000 zikiwa mbioni kuingia katika application hiyo kutoka kwa wasanii mbalimbali na ndipo ilionyesha wasanii Jux, Mbosso, Vanessa Mdee, Nandy, Aslay, Rayvanny na Hermonize kuwa miongoni mwa wasanii waliosikilizwa zaidi barani Afrika.

WASANII Jux na Mbosso anayetoka katika kundi la WCB wamezidi kufanya vizuri katika soko la mziki baada ya nyimbo zao kusikilizwa mara nyingi kupitia katika takwimu za Boomplay za mwaka 2018.

Kwa mwaka jana boomplay ilizalisha nyimbo milioni 833 na takribani nyimbo 30,000 zikiwa mbioni kuingia katika application hiyo kutoka kwa wasanii mbalimbali na ndipo ilionyesha wasanii Jux, Mbosso, Vanessa Mdee, Nandy, Aslay, Rayvanny na Hermonize kuwa miongoni mwa wasanii waliosikilizwa zaidi barani Afrika.

Uteuzi huo umetokana baada ya nyimbo zao kuingia katika 10 bora zilizosikilizwa zaidi ya mara 100 katika orodha ya nyimbo za wasanii wa Tanzania.

Wasanii wengi hivi sasa wamejikita kupeleka nyimbo zao mitandaoni baada ya kuona kwamba ni sehemu nyingine ambayo wanaweza kujizalishia kipato, tofauti na miaka ya nyuma ilikuwa wanategemea shoo tu.

Boomplay inafahamika kuwa chanzo kikubwa cha ukuaji wa muziki katika bara la Afrika na mwaka 2017 iliweza kujinyakulia tuzo ya application bora ya muziki Afrika kupitia kipengele cha ‘’App Afrika Awad’’ ikiwa imewafikiwa watu milioni 38 ulimwenguni kote na milioni 3 kwa Tanzania.

ADVERTISEMENT