In Summary

Mwakani kuna mategemeo ya kuanza kuandaa filamu  kwa kutumia helikopta,kwani sanaa imekuwa na tayari makampuni makubwa yameamua kuithamini  ya filamu nchini

Msanii wa Bongo Movie na muongozaji, Jacob Steven ‘JB’ amefunguka kuhusiana na changamoto wanazozipata katika sanaa ya uigizaji, huku akiwataja wasanii  wengi wameitelekeza sanaa na kuhamia kwenye kazi zingine.

JB ambaye pia mmiliki wa Kamapuni ya kuuza kazi za filamu  ya Jerusalem Film, amesema wasanii wengi wamehamia kwenye biashara ya chakula na wengine kujiingiza kwenye kilimo.

Akizungumza na Mwanaspoti  JB amesema ” Sanaa ya uigizaji Tanzania haithaminiwi sana ndio maana unaona wasanii wengi wanaacha  na kujiingiza kwenye shughuli nyingine. Hata hivyo ndio maana amekuja mkombozi wa sanaa namaanisha ,kampuni ya MP TV ambayo kwa sasa inanunua filamu za Kitanzania na kuziuza katika soko la kimataifa.

Hata hivyo JB amesema mwakani kuna mategemeo ya kuanza kuandaa filamu  kwa kutumia helikopta,kwani sanaa imekuwa na tayari makampuni makubwa yameamua kuithaminisha tasnia yetu ya Bongo Movie.”

ADVERTISEMENT