In Summary

Kazi ya Maua Sama ambayo pamoja na kumpa changamoto ya kukaa rumande kwa muda, imembadilishia maisha yake imempa utajiri ambao unamfanya aendelee kupambana zaidi na kukaa karibu na mashabiki zake.

ACHANA na tukio la kutukanwa kwa nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul kutokana na alichokifanya nchini Kenya kwenda kufanya tamasha lake la Wasafi Festival, inase hii IOKOTE ya mwanadada Maua Sama imefanya maajabu  ya aina yake unaambiwa.
Akizungumza na Mwanaspoti, alisema kazi yake hiyo ambayo pamoja na kumpa changamoto ya kukaa rumande kwa muda, imembadilishia maisha yake imempa utajiri ambao unamfanya aendelee kupambana zaidi na kukaa karibu na mashabiki zake.
Alisema kazi yake hiyo ambayo mbali na kuma fedha ya kununua gari aina ya Rav4 new Model 2017 ambayo ameinunua kwa Sh 80 milion, pia imempa nafasi ya kufanya matamasha mbalimbali ndani na nje ya nchi ambayo yamemuingizia pesa.
"Nawashukuru mashabiki zangu, wao ndio uti wa mgongo wangu bila wao, mimi sio chochote katika kazi, naamini wao ndio wamenifanya nionekane maarufu kupitia kazi hii ninayoifanya nitaendelea kupambana zaidi ili niweze kuendelea kuwafurahisha zaidi,"
"Nimemaliza mwaka vizuri naingia mwaka mpya kwa hari mpya na nguvu mpya nawaahidi mashabiki wa kazi zangu wasitegemee nitawaangusha nitafanya mambo makubwa zaidi ya haya niliyoyafanya ili kuendelea kujitengenezea mazingira ya kuingiza fedha na kujitangaza ndani na nje ya nchi," alisema.

ADVERTISEMENT