In Summary
  • Sasa buana, wakati Simba ‘ikisulubiwa’ kule DR Congo na kuondoshwa katika Ligi ya Mabingwa huku Mazembe wakifuzu kucheza nusu fainali, Ikangaa anakwambia, tangu imeingia hatua ya makundi, mechi ya juzi ndiyo imecheza vizuri.

NANI anasema Simba imefanya vibaya? Licha ya kipigo cha mabao 4-1 kule DR Congo dhidi ya TP Mazembe, bingwa wa zamani wa Afrika wa riadha, Juma Ikangaa anakwambia mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu wamejitofautisha na timu nyingine.

Iko hivi. Simba Juzi Jumamosi ilikubali kipigo hicho katika robo fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya sare ya bila kufungana jijini Dar es Salaam na Mazembe.

Sasa buana, wakati Simba ‘ikisulubiwa’ kule DR Congo na kuondoshwa katika Ligi ya Mabingwa huku Mazembe wakifuzu kucheza nusu fainali, Ikangaa anakwambia, tangu imeingia hatua ya makundi, mechi ya juzi ndiyo imecheza vizuri.

“Kupata bao ugenini! Haijawahi kutokea tangu Simba imeingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa msimu huu,” alisema Ikangaa na kufafanua:

“Pamoja na kwamba wametolewa, lakini imeonyesha mabadiliko, imeweza kupata bao ugenini, kitu ambacho hawakufanya katika mechi zao za makundi, hiyo ni mafanikio makubwa kwa Simba. Lakini pia binafsi nilimuona refa hakuwa ‘fair’ kwa Simba.”

ADVERTISEMENT