In Summary
  • Ripoti kutoka huko Bernabeu zinadai wachezaji wenye majina makubwa katika kikosi hicho wamemfuata Florentino na kumwaambia asajili mshambuliaji mpya.

MADRID, HISPANIA . MASUPASTAA wa Real Madrid wameripotiwa kumfuata rais wa timu hiyo, Florentino Perez na kumtaka afanye usajili wa maana kwa kunasa straika wa nguvu kwenye dirisha hili la Januari.

Kwa sasa kikosi cha Los Blancos kipo nje ya Top Four, huku kikishindwa kabisa kufunga mabao kwenye La Liga na michuano mingine ya msimu huu.

Ripoti kutoka huko Bernabeu zinadai wachezaji wenye majina makubwa katika kikosi hicho wamemfuata Florentino na kumwaambia asajili mshambuliaji mpya.

“Wachezaji wanataka asajiliwe namba 9 kwa sababu Karim Benzema ana matatizo. Hakuna anayependa kuteseka. Amechuja. Na hilo ndilo linalowafanya wachezaji kutaka asajiliwe mshambuliaji mwenye uwezo wa kufunga mabao mengi,” ilibainisha taarifa ya kutoka huko Bernabeu.

“Mchezaji ambaye wengi wametaka asajiliwe ni (Robert) Lewandowski.”

Kuhusu umri imeelezwa wachezaji hao hawakuwa na shida kwani, Ruud Van Nistelrooy alisajiliwa akiwa na umri wa miaka 31 na bado alikwenda kucheza kwa kiwango kikubwa sana kwenye kikosi

hicho.

ADVERTISEMENT