In Summary

 

  • Katika mkataba huo wa mwaka mmoja na kati ya FKF na Kampuni ya Kubeti ya Betin unathamani ya Sh20 milioni itagharamia maandalizi ya timu hiyo, pamoja na ununuzi wa jezi za Stars, pamoja na zile za mashabiki.

Nairobi, Kenya. Kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2019), Timu ya taifa Kenya, Harambee Stars imepata mdhamini mpya, atakayesimamia gharama zote za timu hiyo.

Katika dili hilo la mwaka mmoja, lililosainiwa leo, Kampuni ya Kubeti ya Betin, imeingia mkataba wa Sh20 milioni na Shirikisho la Soka nchini (FKF), dili ambayo itagharamia maandalizi ya timu hiyo, ambapo shilingi 5 milioni, itatumika kugharamia Jezi za Stars, pamoja na zile za mashabiki.

Akizungumza wakati wa uingiaji wa dili hilo, Rais wa Shirikisho la soka nchini, Nick Mwendwa alisema, udhamini huo utasaidia kuwezesha kambi ya Stars, ambayo imepangwa kuwa nchini Ufaransa kwa wiki tatu kabla ya kuelekea Misri.

Mwendwa, alisema dili hilo, linaipatia Betin haki ya kufanya chochote watakachoweza katika kusapoti Harambee Stars, na kuongeza kuwa, huu ni mwanzo tu, kwani kuna dili kibao kama hizo ambazo ziko njiani.

Harambe Stars, inayoongoza Kundi D, itaondoka nchini  machi 22, kuelekea Kumasi, Ghana, kwa ajili ya mechi ya mwisho ya kundi hilo, kufuzu AFCON.

Stars tayari imeshafuzu makala ya 32 ya michuano hiyo itakayofanyika Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 19.

ADVERTISEMENT