In Summary

Gor Mahia ambao ninmabingwa mara mbili mfululizo wa mashindano ya Sport Pesa Cup wamefuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika  wakipangwa kundi  D  na timu ya  Na Hussein Dey ya Algeria,Petro Atletico(Angola) na Zamaleki ya Misri.

Kocha wa Gor Mahia ya Kenya, Hassan Oktay anasema wamekuja Tanzania wakiwa na lengo la kutwaa tena ubingwa wa SportPesa Cup.
Gor Mahia ambao ndio Mabingwa watetezi  wataanza kutupatia  karata ya ya kwanza kesho kwa kuikabiku Mbao katika mchezo utakaoanza saa 8: 00 mchana katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Oktay mwenye uraia wa nchi mbili Uingereza na Uturuki alisema anajua mechi zitakuwa na presha lakini wako  vizuri kiakili na kimbinu kwani wanahitaji kuwa Mabingwa.
"Ukiangalia hatukuwa na muda wa maandalizi ya mashindano haya na leo ndio tumeanza kujiandaa lakini Sina wasiwasi na kikosi Changu kwani tumetoka katika mashindano magumu ya Kombe la Shirikisho Afrika na nashukuru tumeweza kufuzu hatua ya makundi.
"Tumetoka katika mechi ngumu na zimetupa mazoezi mazui, tumekuja Hapa  kucheza kwa uhuru katika mashindano haya ingawa zitakuwa mechi za presha kwani zimekaribiana lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunachukua ubingwa" alisema Oktay.
"Sikuwa na muda wa kuzifuatilia time pinzani lakini najua baada ya Kila mechi tutakuwa Tunawafahamu  zaidi wapinzani wetu"alisema

ADVERTISEMENT