In Summary

Kocha Appiah aliita wachezaji 29  kwenye kikosi chake cha  awali kimejichimbia Abu Dhabi, falme za Kiarabu, anatarajiwa kupunguza  nyota sita, Jumatatu.

Dar es Salaam. Kocha wa timu ya taifa ya Ghana ‘Black Stars’, Kwasi Appiah anatarajia kupunguza baadhi ya nyota wake, Juni 10 ili abakie na wachezaji 23 kuelekea fainali za Mataifa ya Afrika nchini Misri.

Nyota hao 29, walisafiri Jumamosi ya Juni mosi kutoka Ghana kueleka Abu Dhabi ambako wanajifua na kucheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kutua Misri.

Appiah anatajwa kuwa atatumia mchezo wa kirafiki dhidi ya Namibia kuwafanyia tathimini wachezaji wake na baada ya panga kupita watamalizia maandalizi yao Abu Dhabi kwa kujipima ubavu na Afrika Kusini.

Kikosi kamili cha Black Stars kilichopo Abu Dhabi cha wachezaji 29 kinaundwa na makipa, Richard Ofori (Maritzburg United, Afrika Kuisni), Lawrence Ati- Zigi (Sochaux, Montbeliard, Ufaransa), and Felix Annan (Asante Kotoko, Ghana).

Mabeki: John Boye (Metz, Ufaransa), Andy Yiadom (Reading, England), Abdul Baba Rahman (Reims, Ufaransa), Lumor Agbenyenu (Goztepe A.S, Uturuki),  Kassim Nuhu, (Hoffeinham, Ujerumani,) Jonathan Mensah (Columbus Crew SC, Marekani), Joseph Aidoo (Genk,  Ubelgiji ), Nuhu Musa (St Gallen, Usswis), Joseph Attamah (Basaksehir, Uturuki), and Mohammed Alhassan (Hearts of Oak, Ghana)

Viungo, Mubarak Wakaso (Deportivo Alaves, Hispania), Thomas Partey (Atletico Madrid, Hispania), Kwadwo Asamoah (Internazionle, Italia), Ebenezer Ofori (New York FC, Marekani), Afriyie Acquah (Empoli, Italia), Andre Ayew ( Fenerbache, Uturuki).

Wengine ni  Christian Atsu (Newcastle United, England), Samuel Owusu (Cukaricki, Serbia), Thomas Agyepong (Hibernian, Scotland), Yaw Yeboah (Numancia, Hispania),  Abdul Fatawu (Asante Kotoko, Ghana).

Washambuliaji, Asamoah Gyan (Kayserispor, Uturuki), Jordan Ayew (Crystal Palace, England),  Abdul Majeed Waris ( Nantes, Ufaransa), Caleb Ekuban  (Trabzonspor, Uturuki) and Kwabena  Owusu (Leganes, Hispania).

 

ADVERTISEMENT