In Summary

Bielsa alisema hana presha yoyote licha ya kuwakosa nyota wake saba kwa sababu mbalimbali ikiwamo majeruhi na kusimamishwa.

LONDON, England
BOSI wa Leeds United, Marcelo Bielsa amesema wala hajapaniki kwa sasa kutokana na 'ishu' ya usajili, licha ya kikosi chake kuwa na majanga.
Kocha huyo mkongwe alisema pamoja na majanga aliyonayo ya kuwakosa mastaa wake, bado anaamini watapanda Ligi Kuu ya England msimu ujao.
Leeds ipo kileleni kwa sasa katika Ligi Daraja Kwanza England maarufu kama Championship ikiwa na pointi mbili zaidi mbele ya Norwich City, kutokana na michezo yao 26.
Hata hivyo, Bielsa alisema hana presha yoyote licha ya kuwakosa nyota wake saba kwa sababu mbalimbali ikiwamo majeruhi na kusimamishwa.
"Tuna upungufu wa wachezaji," alinukuliwa Bielsa.
"Ikiwa tutaleta wachezaji basi ni lazima wawe bora zaidi kuliko tulionao," alisema.
"Ndani ya wiki chache zijazo, tutakuwa na Dallas, Berardi, Phillips, Brown, Bamford na Douglas kikosini," alisema na kuongeza;
"Kama hatakuja yeyote bado, tuna uwezo wa kutatua matatizo yetu hata hivyo."

ADVERTISEMENT