In Summary

Tanzania imepangwa Kundi C katika fainali za Afcon ikiwa pamoja na Senegal, Algeria na Kenya

Dar es Salaam. Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Credo Mwaipopo amesema nyota wa Taifa Stars wanatakiwa kuonyesha viwango vyao katika fainali za Afcon ilikupata soko katika klabu za Ulaya.

Credo alisema katika fainali hizo kubwa Afrika kumekuwa na mawaka kutoka kila pembe ya dunia ambao husaka vipaji.

Kiungo huyo wa zamani Yanga, alisema wachezaji wa Taifa Stars wanatakiwa kujua kwa Ulaya haya ni majira ya kiangazi ambayo timu nyingi huyatumia kuboresha vikosi vyao kwaajili ya msimu ujao wa 2019/20.

“Nawashauri kuyatizama kwa jicho la tatu mashindano haya, wadogo zangu wakina Msuva, Samatta na wengineo, kupata nafasi kama hii itachukua muda mrefu na umri nao lazima watambue unasogea.

“Naona tunawachezaji wenye vipaji, lakini mawakala wengi hawaamini kwenye Ligi za ukanda wetu hivyo sio rahisi kuja Afrika Mashariki kumfuatilia mchezaji.

“Hili ni jukwaa ambalo wakilitumia vizuri wanaona matunda ya vipaji walivyonavyo Samatta anajua utamu wa soka la Ulaya,” alisema Credo ambaye aliichezea Taifa Stars chini ya Mbrazil, Marcio Maximo.

ADVERTISEMENT