In Summary

Coutinho aliyetua Barcelona akitokea Liverpool, ameshindwa kutamba katika msimu wake wa kwanza na mara kwa mara alikuwa akizomewa na mashabiki wa klabu hiyo ya Nou Camp

Madrid, Hispania. Baada ya kimya cha muda mrefu, Philippe Coutinho amekiri kutokuwa na msimu mzuri katika kikosi cha Barcelona.

Kauli ya nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, imekuja huku kukiwa na tetesi za kutakiwa na Manchester United katika usajili wa majira ya kiangazi.

Coutinho aliyetua Barcelona akitokea Liverpool, ameshindwa kutamba katika msimu wake wa kwanza na mara kwa mara alikuwa akizomewa na mashabiki wa klabu hiyo ya Nou Camp.

Nyota huyo mwenye miaka 26, alidokeza anatafakari mchango wake ndani ya Barcelona kabla ya kuchukua uamuzi.

Pamoja na kufanya vibaya Barcelona, nyota huyo amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Brazil kwenye mechi za kujiandaa na Fainali za Copa Amerika.

“Sikuwa na msimu mzuri, kiwango changu kilikuwa na changamoto kubwa. Lakini njia pekee ni kupambana kufanya kazi kwa nguvu, naamini ninaweza,” alisema Coutinho.

Mshambuliaji huyo amekuwa na presha kubwa kutoka kwa mashabiki kwa kuwa alinunuliwa kwa bei mbaya na kuweka rekodi katika usajili wa klabu hiyo.

ADVERTISEMENT