In Summary

Ripoti zinadai kwamba Conte mpango wake ni kurudi tena kwenye Ligi Kuu England au kunoa timu yoyote ya Italia katika kibarua chake kijacho kwenye ukocha. Kocha huyo ndoto zake ni kuinoa Juventus au Manchester United.

MILAN, ITALIA. KOCHA, Mtaliano Antonio Conte kwa sasa yupo tu kijiweni, hana kazi.

Taarifa zinadai kwamba Conte yupo tayari kuchukua kazi nyingine yoyote, lakini sio kwenda kuinoa Real Madrid.

Mwanzoni wakati anafutwa kazi huko Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita, Conte alikuwa akuhusishwa na mpango wa kwenda kuchukua kazi huko Santiago Bernabeu. Lakini, kwa sasa kazi hiyo haitaki kabisa.

Ripoti zinadai kwamba Conte mpango wake ni kurudi tena kwenye Ligi Kuu England au kunoa timu yoyote ya Italia katika kibarua chake kijacho kwenye ukocha. Kocha huyo ndoto zake ni kuinoa Juventus au Manchester United.

Conte yupo makini kufuatilia maendeleo ya Ole Gunnar Solskjaer huko Man United, lakini akitazama pia uwezekano wa kurejea Juventus, ambako kocha wa sasa Max Allegri anadaiwa kwamba huenda akaachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu kwenda kuchukua kazi ya kuinoa Real Madrid.

ADVERTISEMENT