In Summary

Chirwa alijiunga na Azam FC msimu uliopita na kufanikiwa kuipa nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho baada ya kuifungia bao 1-0 katika mchezo wa fainali dhidi ya Lipuli.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Azam FC, Obrey Chirwa amefunguka sababu za kushindwa kutimiza ahadi yake ya kufunga mabao 10 msimu uliopita ni kukamiwa na mabeki.

Chirwa ameongeza mkataba wa kuitumikia Azam FC kwa msimu mpya wa ligi alisema soka linamambo mengi mtu anaweza kuweka ahadi na asitimize kutokana na ushindani ikiwa ni sambamba na baadhi ya wachezaji kuwakamia.

Alisema malengo yake ya kuhakikisha anaipambania timu yake hiyo yapo palepale mbali na changamoto anazokutana nazo kila anapokuwa katika mapambano na kuongeza kuwa ahadi huwa aifutiki ivyo msimu ujao atafanya makubwa zaidi ya aliyoyafanya msimu ulioisha.

"Unajua kuna muda mtu unaweza kuonekana hakuna unachokifanya uwanjani kutokana na kupewa changamoto ya kukabwa na walinzi zaidi ya watatu kubwa hawataki kuona unawafunga jambo hilo lilinikuta msimu ulioisha."

"Niliahidi kufunga bao kumi katika mkataba wa mwaka mmoja niliokuwa nimesaini dirisha dogo la usajili, lakini nilishindwa kufanya hivyo kutokana na kukamiwa na mabeki lakini naomba kuahidi kuwa hilo halijanikatisha tamaa nitaendeleza mapambano msimu unaokuja," alisema Chirwa.

ADVERTISEMENT