In Summary

Banka alijiunga na Yanga akitokea Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka miwili hakuwa na msimu mzuri kutokana na kukosa namba katika kikosi cha kwanza cha Mwinyi Zahera.

Dar es Salaam. Kiungo wa Yanga, Mohamed Issa 'Banka' amesema kocha Mwinyi Zahera ashindwe mwenyewe sasa kwani safu ya kiungo imekamilika na kumwagia sifa Abdulaziz Makame kwamba uongozi umelamba dume kupata saini yake.

Banka hakuwa na msimu mzuri msimu uliopita kutokana na kukosa namba kikosi cha kwanza cha Zahera, lakini amesema Makame ni kiungo mzuri akipata wachezaji wenye kasi basi timu pinzani waandike maumivu.

Alisema uwepo wa Feisal Salum 'Fei Toto' yeye mwenyewe na Makame umekamilisha safu ya kiungo ya timu ya taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Herous' na kuweka wazi kuwa endapo siku kocha wao atawapa nafasi ya kucheza pamoja basi moto utawaka.

"Utatu wetu huo tunafahamiana tunajua mipira gani tukipiga inamfikia mtu kwa wakati lakini uchezaji wa Makame ni wa tofauti kidogo yeye anaweza kupiga mipira mirefu mifupi na kwenye suala la faulo ndio kiboko uongozi haujakosea kufanya maamuzi ya kumpa mkataba."

"Nafurahi kuona tunacheza pamoja timu moja na natamani siku nipewe nafasi ya kucheza na nyota hao ili kuweza kutengeneza umoja ambao naamini ni wewngi wanatamani kuuona na naamini hatuwezi kumuangusha mwalimu," alisema Banka.

ADVERTISEMENT