Dar es Salaam. Polisi jijini Dar es Salaam wamesema kwamba wanamsaka mwanaume aliyeonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa na msanii maarufu Wema Sepetu.

Akizungumza na jijini Dar es Salaam leo Novemba 6 Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Liberatus Sabas amesema kwamba polisi wanaendelea kumsaka mwanaume huyo na wakimpata wanamfikisha mahakamani.

“Polisi tunaendelea kumtafuta huyu jamaa hatujaakata tamaa na ikiwa tutamkamata lazima tumfikishe mahakamani kwani ana kesi ya kujibu,’’ amesema.

Amesema kwamba watu wanadhani labda jeshi la polisi limeshaachana na mwanaume huyo lakini bado ni mtuhumiwa na hivyo akikamatwa anapelekwa mahakamani.

ADVERTISEMENT