In Summary

Msani wa muziki wa kizazi kipya, AliKiba ameweka wazi sababu za kuchelewa kutoa nyimbo mpya wakati nyimbo zingine zinaendelea kufanya vizuri sokoni.


MWANAMUZIKI wa Bongo fleva, Ali Kiba ametoa sababu  ya kuchelewa kutoa nyimbo mpya kama wanavyotaka mashabiki zake huku akimshukuru Mungu kuongeza familia baada ya kupata wa kiume na mke wake Amina.
Katika mahojiano yake na kipindi cha XXL kinachorushwa na kiruo cha redio Clouds, Kiba amesema hataki kutoa wimbo ambao haujamuingizia faida sababu muziki ni biashara.
Kiba anasema kama bidhaa yake ya muziki inafanya vizuri sokoni hana sababu ya kutoa wimbo mwingine kwani akifanya hivyo ataua bidhaa iliyopo sokoni.
“Unajua watu wanachoshindwa kunielewa ni hapa, mimi sitaki kutoa wimbo kabla mwingine haujaniingizia faida, najua kabisa muziki ni biashara, kama bidhaa yangu inafanya vizuri sokoni  sina sababu ya kutoa wimbo mwingine maana itaua bidhaa iliyopo sokoni, ndio maana nakaa muda mrefu kutoa wimbo mpya,” anasema
Kiba anasema kwa sasa amejifunza kucheza na msimu kwani msanii akipotea mara ya kwanza na akipotea mara pili ni kitendo cha kujimaliza kisanii ndiyo maana katika nyimbo zake hawezi kupita njia ambayo alipita katika nyimbo zilizopita.
Akizungumzia upande wa familia yake, anasema "Namshukuru Mungu kuongeza familia kwa kupata mtoto wa kiume na mke wangu Amina, hii ni baraka kubwa kutoka kwa Mungu,"

ADVERTISEMENT