In Summary
  • Timu Sita  zinachuana kumsaka mbabe wa Wilaya ya Ilemela ambapo pia klabu tatu zitakazokuwa na pointi nyingi ndizo zitakazopanda Daraja la Tatu mkoa Mwanza

AFRICAN Boys imeanza vyema hatua ya Sita Bora ya Ligi Daraja la Nne Wilaya ya Ilemela baada ya juzi kuwabamiza Jock Boys mabao 3-1 kwenye mtanange uliopigwa uwanja wa Nyamagana jijini hapa.

Katika mpambano huo, African Boys walipata bao la kuongoza lililowekwa nyavuni na straika wao Pamba Yohana dakika ya 22 kipindi cha kwanza huku Jock Boys wakisawazisha bao hilo dakika ya 30 lililofungwa na Amossi Wayalla.

Kipindi cha pili ,African Boys waliendeleza makali yao na kupata bao la pili lililowekwa kambani na Juma Kijiko dakika ya 50.

Wakati Jock Boys wakitafakari namna ya kusawazisha bao hilo walijikuta wakipachikwa la tatu dakika ya 58 lililopachikwa na Selemani Shedrack.

Kocha African Boys, Ernest Renatus aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo ambapo amesema sasa kwake kile mechi wanayocheza ni mwendo wa kugawa dozi.

“Tumejipanga msimu huu na lengo letu kubwa ni kupanda Daraja la Tatu Ngazi ya Mkoa Mwanza hivyo sasa kile mchezo kwetu ni kupata pointi tatu”alisema Renatus.

ADVERTISEMENT