In Summary

Katika mazoezi hayo AS Vita ilianza kupasha misuli kwa kukimbia nusu uwanja na baada ya hapo walifanya mazoezi yao ambayo waliyagawa kwa dakika.

Dar es Salaam. Nyota wa AS Vita wametumia dakika 60 kujifua kwenye Uwanja wa Gymkhana tayari kwaajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabigwa Afrika Afrika dhidi ya wenyeji Simba Jumamosi kwenye Uwanja Taifa.

Katika mazoezi hayo AS Vita ilianza kupasha misuli kwa kukimbia nusu uwanja na baada ya hapo walifanya mazoezi yao ambayo waliyagawa kwa dakika.

Wameanza kwa kupasiana pasi za haraka haraka, wakagawa timu mbili kwa kuchezeshwa na viungo na mawinga, mipira mirefu ambayo ilikiwa ikipigwa na kipa ili mabeki wanne kuzuia washambuliaji wasipachike mabao, mwengine mabeki kukaba washambuliaji na baadaye pasi kuchongwa na mabeki ili iwafikie washambuliaji.

Wachezaji walicheza kwa pasi fupi fupi zilizokuwa zinafika kwa muhusika huku kila mmoja akiwa anamkaba mwenzake bila kumpa nafasi ya kuchezea mpira.

Mara baada ya kumaliza mazoezi yote hayo matano tofauti kocha Florent Ibenge ilipuliza kipyenga cha mwisho ili wachezaji wake kumaliza mazoezi.

Baada ya kumaliza walikusanyika nje ya uwanja ambapo walipumzika kwa muda mfupi kabla ya kuweka duara kisha kufanya maombi na kuanza safari ya kurudi hotelini kwao.

ADVERTISEMENT