In Summary

Enzi za uhai wake Mrisho alitamba akiwa katika kikosi cha Yanga pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’

Dar es Salaam. Mwili wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Said Mrisho ‘Zico wa Kilosa’ amefariki akiwa njia kuletwa hospitalini Dar es Salaam utazikwa kesho nyumbani kwao Kilosa, Morogoro.

Mrisho alifariki leo mchana akiwa njiani kuletwa hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam kwa matibabu baada ya kusumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Mwenyekiti wa Umoja wa wanasoka Veterans Nchini (UMSOTA), Paul Lusozi (Faza Lusozi) alisema Mrisho ameaga dunia wakiwa katika harakati za kumpeleka katika matibabu Muhimbili.

"Nilienda kumchukua Morogoro ili kumleta Muhimbili kwa matibabu, kwa ari aliyokuwa nayo hakuweza kupanda basi, tulitafuta gari ya wagonjwa (Ambulance) tukapata, lakini kabla hatujaondoka Morogoro ikaharibika.

"Ilibidi mimi nirudi Dar na ndugu zake wakafanya mchakato wa kukodi Noah ili wamlete, umoja wetu ambao ndiyo tulikuwa tunagharamia matibabu yake tumpokee Dar es Salaam, walifanikiwa na sisi tulikuwa Muhimbili tukiweka taratibu sawa kwa ajili ya matibabu yake, lakini bahati mbaya walipofika Mikese alikata roho," alisema Faza Lusozi.

Alisema gari iliyokuwa ikimleta Dar es Salaam iligeuzia Mikese na kwenda Morogoro kuchukua ndugu kwa ajili ya kuwapeleka Kilosa kwenye mazishi yatakayofanyika kesho Jumatano.

ADVERTISEMENT