In Summary

Kwa mabeki hao wa kati wa Taifa Stars, Morris  ni mkubwa kidogo kwa  Yondan pamoja na kuwa wote wamezaliwa mwaka 1984, ukubwa wake unatokana na kupishana kwao miezi ya kuzaliwa na siku.

Dar es Salaam. Mabeki wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Kelvin Yondani na Agrey Morris ni wachezaji mwenye umri mkubwa zaidi kati katika timu za Kundi C katika fainali za mataifa ya Afrika.

Kwa mabeki hao wa kati wa Taifa Stars, Morris  ni mkubwa kidogo kwa  Yondan pamoja na kuwa wote wamezaliwa mwaka 1984, ukubwa wake unatokana na kupishana kwao miezi ya kuzaliwa na siku.

Morris ambaye amekuwa katika kiwango bora kwa muda mrefu, alizaliwa Machi 12, huku Yondani akizaliwa miezi saba baadaye ambapo ilikuwa Oktoba, 9 mwaka huo.

Wanaokaribia umri wa mabeki hao shupavu wa Yanga na Azam ni kiungo wa Sofapaka, Dennis Odhiambo atakayeichezea Kenya.

Odhiambo ameiwezesha Sofapaka kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Kenya, amezidiwa zaidi ya miezi 10 na Yondani kutokana na kuzaliwa kwake Machi 18, 1985.

Mwengine ni nyota wa timu ya taifa ya Algeria, Adlane Guedioura wa Nottingham Forest ya England aliyezaliwa Oktoba 20, 1989.

Kwenye kikosi cha Senegal wenye umri mkubwa ni wachezaji wanne ambao ni Saliou Cisse (Valenciennes/Ufaransa), Idrissa Guaye (Everton/ England), Cheikhou Kouyate (Crystal Palace/England) na Lamine Gassama (Goztepe Spor Kulubu/ Uturuki) wote hao wamezaliwa 1989.

ADVERTISEMENT