In Summary

Golden Eaglets wakiwa na Akande wakutacheza na timu ya taifa ya Tanzania yenye umri chini ya miaka 17 kwenye mchezo wa ufunguzi wa mataifa ya Afrika kwa vijana (U17), Aprili 14-28.

Dar es Salaam. Kinda wa Chelsea, Adrian Akande amepewa jezi namba 10 kwenye kikosi cha vijana cha Nigeria chini ya umri wa miaka 17 ‘Golden Eaglets’ ambacho kitashiriki fainali ya mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza Tanzania.

Kupewa jezi namba 10 kwa Akande kumezua mijadala Nigeria kwa kuanza kuzungumzwa kuwa huenda kinda huyo akafuata nyayo za John Obi Mikel, Wilson Oruma, Kelechi Iheanacho na Kelechi Nwakali.

Wakali hao wa Nigeria kwa vipindi tofauti waliwahi kuivaa jezi hiyo hivyo aliyopewa Akande mwenye mabao 30 kwenye timu ya vijana ya Chelsea, anaweza kuwa msaada kwenye taifa hilo kwa siku za usoni.

Nyota wa zamani wa Chelsea, Mikel aliuvaa uzi huo wenye namba 10 mgongoni  2003 kwenye kombe la dunia na kiungo wa zamani wa Marseille, Wilson Oruma, aliuvaa na kuibuka mfungaji bora wa kombe la dunia, 1993 akiwa na mabao sita.

Wachezaji bora wa kombe la dunia kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kwenye misimu miwili tofuati 'Golden Ball winners', Kelechi Iheanacho (2013) wa Leicester City na Kelechi Nwakali (2015) wa Arsenal nao walivaa jezi namba 10.

Kocha  wa kikosi cha Golden Eaglets,  Manu Garba alidai kuwa kikosi chake atakijenga kwa kuzunguka winga huyo katika michuano ya kombe la dunia la vinajana kama wakipata nafasi hiyo.

Kikosi kamili cha Golden Eaglets kilichotua nchini kushiriki Afcon U17 ni Sunday Stephen, Shedrack Tanko, Ogaga Oduko, Samson Okikiola Tijani, Clement Chigozie Ikenna, David Akulo Ishaya, Olakunle Junior Olusegun.

Mayowa David Abayomi, Wisdom Ubani, Adrian Akande, Mubaraq Gata Adeshina, Shuaib Abdulrazaq, Akinkunmi Ayobami Amoo, Olatomi Alfred Olaniyan.

Wengine ni Charles Etim, Suleman Shaibu, Peter Agba, Divine Nwachukwu, Ibraheem Olalekan Jabaar, Fawaz Abdullahi, Ayomide Oluwabusola.

ADVERTISEMENT