In Summary

Beki wa Simba, Zana Coulibaly amekosa penalti kwenye mchezo wa nusu fainali wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi lakini ameonekana kuwa na furaha kubwa baada ya kuungana na mashabiki wao kushangilia.

Simba imeshinda penalti 3-1 dhidi ya Malindi ambapo Zana alikuwa mpigaji wa kwanza upande wa Simba.

Tangu ajiunge Simba kutoka Ivory Coast amekuwa kivutio ndani ya timu hiyo kwani timu yake ikishinda mara nyingi huwa anashangilia kwa kucheza.

Zana alisema "Nimefurahi sana kuingia hatua hii ingawa nasikitika nimekosa kufunga penalti, lakini kukosa kwangu hakunifanyi nishindwe kushangilia na kufurahi.

"Huu ushindi ni wetu sote naamini hata fainali tutafanya vizuri na kuchukuwa ubingwa," alisema Zana.

ADVERTISEMENT