In Summary

Tayari Azam wao wamefuzu hatua ya fainali itakayochezwa keshokutwa Jumapili kisiwani Pemba baada ya kuifunga KMKM bao 3-0 mechi iliyochezwa jioni ya leo Ijumaa.

DAKIKA 45 za kipindi cha kwanza zimemalizika huku si Simba wala Malindi ambayo imeona lango la mwenzake katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi inayochezwa uwanja wa Amaan kisiwani hapa.

Tayari Azam wao wamefuzu hatua ya fainali itakayochezwa keshokutwa Jumapili kisiwani Pemba baada ya kuifunga KMKM bao 3-0 mechi iliyochezwa jioni ya leo Ijumaa.

Mshindi atakayepatikana katika mchezo huu wa Simba na Malindi ndiye atakayecheza na Azam ambao ndiyo mabingwa watetezi wa kombe hilo.

Katika dakika 45 za mwanzo Simba ilifanya mashambulizi lakini safu yao haikuwa makini katika umaliziaje baada ya Adam Salamba kukosa nafasi nyingi.

Dakika ya 21, DicksonĀ  Mlilu wa Simba naye alikosa bao baada ya shuti lake kutoka nje ya goli huku Mohamed Rashid naye akipaisha dakika ya 22.

Simba iliendelea na mashambulizi ya mara kwa mara ambapo dakika ya 34, Asante Kwasi alifunga bao lakini mwamuzi Farhan alikataa kwa madai kwamba aliitwa.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko zilitoka suluhu ya kutofungana.

ADVERTISEMENT