In Summary

Hamisa Mobetto amesema, tangu aachane na Diamond Platinumz amekuwa akipiga 'dili' za maana zaidi ikiwa ni matangazo jambo lililomfanya ashangae kwani ni tofauti na alivyokuwa na mwanamuziki huyo.

 Dar es Salaam. Tangu mrembo, Hamisa Mobetto aachane na mzazi mwenzake, Abdul Naseeb 'Diamond Platinumz' amekuwa akipiga pesa ndefu kutokana na 'dili' anazopa hadi mwenyewe anashangaa.

Mobetto ambaye kwa sasa na Diamond wamebaki kutunza mtoto wao lakini mahusiano ya kimapenzi walishamaliza na sababu kubwa ikidaiwa ni sauti zilizodaiwa ni maongezi yake na mganga wa kienyeji.

Sauti hizo zilidaiwa kuwa Mobetto alikwenda kwa ajili ya kumfunika Diamond aachane na wanawake wake wote na afunge ndoa mrembo huyo.

Amesema, tangu aachane na  mwanamuziki huyo 'dili'  nyingi zimekuwa zikimwangukia hasa za matangazo wakati hapo nyuma haikuwa hivyo na anaona kama ameondoa gundu lililokuwa linamzibia riziki.

“Unajua sasa hivi ninapata 'madili' mengi hadi mimi mwenyewe nashangaa baraka zote hizi zilikuwa wapi tangu mwanzo. Mbona nilikuwa sipati. Yaani utadhani nilikuwa na mtu ambaye alikuwa ananipa gundu (mkosi) lakini sasa baada ya kumkwepa ndiyo limenitoka,” alisema Hamisa.

Mobetto ambaye siku chache zilizopita alinunulia gari jipya aina ya Toyota Vaguard baada ya ile ya awali aina ya Toyota Rav 4 aliyonunuliwa na Diamond aliposhika ujauzito wake.

ADVERTISEMENT